Ijumaa , 10th Apr , 2015

Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva nchini ulioanza leo baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT

Waziri wa Kazi na Ajira Mhe. Gaudencia Kabaka amefanikiwa kumaliza mgomo wa madereva nchini ulioanza leo baada ya kutangaza kufuta agizo lililokuwa likiwataka madereva wa mabasi na malori kwenda kusoma tena katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

Akiongea baada ya kikao kilichofanyika katika kituo Kikuu cha Mabasi cha Ubungo, Mhe. Kabaka amesema mbali na kufuta agizo hilo, pia aprili 18 ataitisha mkutano utakaoikutanisha Wizara yake, Wazara ya Uchukuzi pamoja na viongozi wa madereva hao.

Awali polisi Jijini Dar es Salaam walilazimika kutumia mabomu ya machozi katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo kutuliza vurugu zinazofanywa na kundi la watu wakiwemo madereva, abiria pamoja na wananchi kufuatia mgomo wa madereva.

Mgomo huo, ambao mbali na kuwaathiri wasafiri wa kwenda mikoani na nje ya nchi pia uliwaathiri watumiaji wa usafiri wa daladala katika baadhi ya mikoa, wakiwemo wakazi wa Dar es Salaam.