JPM ateua Kamishna wa Madini na bosi wa PURA

Friday , 21st Apr , 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Mhandisi Benjamin Joel Mchwampaka kuwa Kamishna wa Madini.

Rais Magufuli

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Benjamin Joel Mchwampaka umeanza tarehe 19 Aprili, 2017.

Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Benjamin Joel Mchwampaka alikuwa Kamishna Msaidizi sehemu ya uchimbaji mdogo wa madini.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Adelardus Kilangi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli (Petroleum Upstream Regulatory Authority - PURA).

Dkt. Adelardus Kilangi ni Mkurugenzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino Tanzania (SAUT) kampasi ya Arusha.
Uteuzi wa Dkt. Adelardus Kilangi umeanza tarehe 19 Aprili, 2017

Recent Posts

Current Affairs
Rais Mugabe atumbuliwa

Msanii Irene Uwoya.

Current Affairs
Uwoya otokwa povu kisa mtoto

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.

Current Affairs
Serikali kuvunja nyumba zilizojengwa bila kibali