Jumatatu , 7th Feb , 2022

Watoto wawili wa familia moja katika kijiji cha Usuhilo Manispaa ya Tabora, wamefariki dunia kwa kukosa hewa ya kutosha baada ya wazazi wao kuwasha jiko la mkaa na kuliweka ndani ili waote moto na kuikinga na baridi.

Jiko la mkaa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema kwamba kutokana na nyumba waliyokuwa wakiishi familia hiyo ya watu watano kuwa na madirisha madogo ilipelekea kukosa hewa na wawili kufariki huku wengine wakikimbizwa hospitali kwa mataibabu.

Katika tukio hilo watu watatu wakiwemo Baba na Mama wa watoto hao bado hali zao si nzuri na wamelazwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete.