Jumapili , 18th Mei , 2014

Mwenyekiti wa bodi ya kampuni ya usafiri jijini Dar es salaam UDA Bwana Robert Kisena amesema hisa za serikali katika kampuni hiyo ziko salama.

Mwenyekiti wa bodi ya UDA Bwana Robert Kisena

Hisa za serikali katika kampuni ya usafiri jijini Dar es Salaam (UDA) ambazo ni asilimia 23 zipo salama na zimekuwa zikiongezeka thamani yake kila siku.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa UDA Bw. Robert Kisena wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa hisa za shirika hilo pamoja na kuelezea wamiliki wake.

Aidha Bw. Kisena amekiri kwamba baadhi ya madereva wa UDA wamekuwa wakikatisha ruti pamoja na kutoa lugha chafu kwa abiria na kusema kwamba suala hilo kwa sasa linashughulikiwa na ndani ya wiki mbili zijazo litakuwa limemalizwa.