Jumatano , 23rd Sep , 2020

Mgombea wa Ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)  katika jimbo la Tanga mjini Ummy Mwalimu, amesema kuwa uwezeshaji wa kiuchumi ni moja ya kipaumbele chake endapo atachaguliwa kuongoza jimbo hilo.

Ummy Mwalimu

Akizungumza na wananchi wa kata ya  Mzizima, Ummy, ameahidi kusimamia uwezeshaji wa kiuchumi kwani utasaidia katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wake 

"Nitasimamia uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake, vijana watu wenye ulemavu pamoja na wajasiriamali wadogowadogo ndugu zangu wana mzizima hiko ndicho kipaumbele changu cha kwanza” amesema Ummy Mwalimu

Aliendelea kufafanua, “Ninaamini tukiwa na kipato cha uhakika hata masuala ya elimu kwa watoto wetu yatakuwa yamepatiwa ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili".