Jumatano , 9th Mar , 2016

Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa amesema Jumuiya ya Afrika mashariki imejikita katika kuimarisha masuala ya uchumi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya reli, barabara, Usafiri wa majini vitu ambavyo vitachochea kasi ya maendeleo kwa nchi wanachama.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa tano kikao cha nne cha bunge la tatu la Afrika Mashariki,Waziri Mkuu amesema nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki zimeweza kukuza pato lake baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya fursa vya kibiashara.

Waziri Mkuu Majaliwa amelitaka bunge hilo lifanye mapitio katika kuboresha uondoaji wa vikwazo vya kibiashara na kufanya sekta binafsi ziweze kushiriki moja kwa moja katika biashara ndani ya jumuiya hiyo.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa kimataifa, Kikanda na Afrika Mashariki, Balozi Agustino Mahiga, amesema kuwa utengamano wa Afrika mashariki ni vizuri zaidi ukaelekezwa kwa kuinua uchumi Kwa wanachama kwa kutegemea zaidi biashara.

Nae Mbunge wa Jumuiya hiyo kutoka nchini Tanzania, Shyrose Bhanji ametaka utengamani wa jumuiya hiyo uwekwe zaidi kwa wananchi wa nchi wananchama badala ya viongozi kama ilivyosasa.