Jumamosi , 2nd Dec , 2017

Chama cha Mapinduzi CCM kimeweka wazi sababu iliyowafanya wakatae kumpokea msanii Wema Sepetu kwenye chama hicho, ambaye hapo jana ametangaza kurudi kundini.

Akizungumza na mwandishi wa East Africa Television, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, kwanza amekanusha kumpokea mwanachama huyo na kusema kwamba, hakufuata utaratibu sahihi kuweza kurejea kwenye chama hicho ambacho alikiasi.

Pole Pole ameendelea kwa kusema kwamba CCM inajidhatiti katika kujijengea misingi imara na wanachama wake, hivyo wanataka mtu ambaye anaenda CCM awe amejidhatiti, kwani hawataki kuja kubeba mizigo ya lawama. 

Pamoja na hayo Polepole amekanusha taarifa zilizosambaa mitandaoni kwamba msanii huyo ameshawishiwa kurudi CCM baada ya kuahidiwa atasaidiwa kumaliza kesi yake inayomkabili mahakamamni, pamoja na kunusuru kubomolewa kwa nyumba yao. 

Msikilize Pole pole hapa.