Wakili wa Oscar Amhoji Shahidi
Wakili wa Utetezi wa mwanaridha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius leo ameanza kumhoji jirani wa mteja wake aliyeiambia mahakama jana kuwa alisikia mwanamke akipiga mayowe na kuomba msaada siku ya tukio la mauaji Februari 14, 2013.