Afrika Mashariki yatakiwa kudhibiti fedha haramu

Nchi za Afrika Mashariki zipo hatarini kuzuiwa kufanya biashara na Marekani iwapo hazitatumia mfumo na sheria za Marekani katika kukabiliana na fedha haramu na uhalifu katika sekta ya fedha.

Mshauri wa masuala ya fedha kutoka taasisi ya Deloitte Bw. Robert Nyamu, ameyasema hayo jijini Dar es Salaam leo, wakati akitoa ripoti ya hali ya uhalifu katika sekta ya fedha kwa nchi za Afrika Mashariki, ambapo Tanzania imeonekana kuongoza kwa wizi wa fedha unaofanywa kwa njia ya unyang'anyi.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS