Kamati ya Maridhiano yatafuta muafaka wa kanuni

Semina ya kujadili Kanuni za Bunge Maalum la Katiba nchini Tanzania imeahirishwa leo mchana hadi kesho asubuhi, ili kutoa fursa ya kwa Kamati ya Mashauriano na Maridhiano kupata muafaka wa vifungu vya kanuni vilivyoligawa bunge hilo, kikiwemo kile cha namna ya upigaji kura iwapo uwe wa wazi ama siri.

Mwenyekiti wa Muda wa bunge Maalum la Katiba, Pandu Ameir Kificho, amechagua wajumbe mbalimbali waliounda kamati hiyo na kuanza kujadili vifungu hivyo namba 39 hadi 43, kazi ambayo wameianza muda mchache uliopita ili kufikia maridhiano.

Pages

Subscribe to East Africa Television RSS