Bunge Maalum la Katiba lapitisha kanuni zake
Baada ya siku 21 za malumbano juu ya kanuni zitakazoliongoza Bunge Maalumu la Katiba nchini Tanzania, leo wajumbe wa bunge hilo wameridhia kuipitisha kanuni, isipokuwa vifungu namba 37 na 38 ambavyo vinazungumzia utaratibu wa upigaji kura.