Kamati ya sheria TFF yaigomea Simba
Kamati ya Sheria na hadhi za Wachezaji ya shirikisho la la soka nchini Tanzania TFF, imekutana Machi 30 mwaka huu kujadili utekelezaji wa maagizo ya TFF kwa wanachama wake, ikiwa ni pamoja kurekebisha Katiba zao ili ziendane na Katiba ya TFF pamoja na ile ya FIFA kabla ya Machi 30 mwaka huu.
Kamati hiyo imekatakaa pendekezo la wanachama wa Simba kubadili kipengele na 26 kuhusu sifa za mgombea ambacho kilikuwa kinazuia mgombea ambaye ametumikia kifungo kutogombea kinapingana na kipengele na 29 (4) cha Katiba ya TFF