Wanachama Simba waonywa kuhusu kampeni za mapema
Uongozi wa klabu ya soka ya simba ya jijini Dar es salaam umewataka wanachama wake wote wanaotaraji kuwania uongozi ndani ya klabu hiyo katika uchaguzi utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao kufuata taratibu na sheria za uchaguzi wa klabu hiyo.