Umati wa watu waahirisha mkutano wa Lowassa Tanga
Mkutano wa kampeni ya mgombea urais kupitia chama CHADEMA, Edward Lowassa umeahirishwa mara baada ya wananchi kujitokeza kwa wingi kumsikiliza hali iliyopelekea baadhi ya wananchi kupoteza fahamu kwa kukanyagana uwanja wa Tangamano jijini Tanga.