Kipindupindu chavamia jiji la Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha mjini, Fadhili Nkurlu, amepiga marufuku uuzwaji wa vyakula katika mazingira machafu, matunda na vimiminika vingine kwa muda usiojulikana, kutokana na ugonjwa wa kipindupindu kuingia wilayani humo.