Serikali yatakiwa kusimamia mazingira na maliasili
Wanafunzi wanaojihusisha na utunzaji wa mazingira nchini Tanzania na Sweden wameiomba serikali kutunga sheria kali zitakazotekelezwa ili kudhibiti tatizo la uharibifu wa mazingira na mauaji ya wanyamapori yanaoyoendelea hapa nchini.

