Monday , 28th Dec , 2015

Wanafunzi wanaojihusisha na utunzaji wa mazingira nchini Tanzania na Sweden wameiomba serikali kutunga sheria kali zitakazotekelezwa ili kudhibiti tatizo la uharibifu wa mazingira na mauaji ya wanyamapori yanaoyoendelea hapa nchini.

uharibifu wa mazingira katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Iringa

Wanafunzi hao wapo nchini kwa ajili ya kufanya majaribio ya kutumia takataka na chupa za plasitiki kuzalisha nishati ambayo itatumika mashuleni kwa ajili ya kupikia ili kupunguza matumizi ya kuni ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira.

Mmoja wa wanafunzi hao akizungumzia suala zima la mauaji ya wanyamapori ambapo amesema licha tu ya kupunguza vivutio vya utalii lakini pia nchi inakosa mapato kutokana na hali hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Mt. Melgoreth, Sista Lucia Njau amesema kuwa shule yake imeanza kunufaika na majaribio yanayofanywa na wanafunzi hao ambapo kwa sasa wanatumia nishati inayotengenezwa na umeme wa chupa za plasitiki.

Naye mtaalamu wa masuala ya mazingira amesema endapo jamii itazingitia utunzaji wa mazingira basi nchi itaweza kukabiliana na majanga yanayotokana na mabadiliko ya tabia nchi.