12 washikiliwa na Polisi ubadhirifu mali ya Umma
Jeshi la Polisi nchini linawashikilia maafisa 12 wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa tuhuma za utoroshwaji wa makontena 349 bandarini kufuatia uchunguzi uliofanywa na wataalam waliobobea katika uchunguzi wa makosa ya uhalifu wa kifedha wa jeshi hilo.