Mshindi wa Airtel Trace Music Stars kuondoka kesho
Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, leo imemkabidhi Bendera ya Taifa, mwanadada Melisa John ambaye ndiye mwakilishi wa Tanzania kwenye Shindano la Airtel Trace Music Stars litakalofanyika jijini Lagos nchini Nigeria na kuhusisha nchi tisa.