Wizara yafafanua sifa za kujiunga na elimu ya juu
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi imetoa ufafanuzi juu ya mfumo wa kujiunga na masomo ya elimu ya juu baada ya kuenea kwa taarifa za upotoshaji kuhusu mchakato wa kujiunga na masomo hayo.

