Wamachinga waachwe mjini - Rais Magufuli
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo (Machinga) katika jiji la Mwanza.

