CHADEMA yatinga kortini kutaka Lema ashtakiwe
Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema, John Mallya, amesema chama hicho kimefungua kesi Mahakama Kuu kutaka Mbunge wa Arusha Mjini, Mh. Godbless Lema, afikishwe Mahakamani baada ya kukaa Mahabusu kwa muda wa siku 6 kinyume cha sheria.