Serikali kufuta utitiri wa kodi kwenye viwanda
Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali inajipanga kuondoa utitiri wa kodi mbalimbali zinatozwa kwenye viwanda kama hatua ya kuviwezesha viwanda vingi nchini kuongeza uzalishaji na kutoa ajira nyingi kwa watanzania.