TFF yasikitishwa na kashfa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesikitishwa na kauli iliyotolewa na mlinda mlango wa timu ya Shupavu ya Morogoro Halifa Mgwira ya kudai wamefungwa na Azam FC 5-0 kutoka na kutopewa pesa ya chakula na Shirikisho hilo.