Msanii Radio wa Uganda afariki dunia
Msanii maarufu kutoka Uganda Moses Ssekibogo, maarufu kama Mowzey Radio amefariki dunia mapema leo asubuhi akiwa katika hospitali ya CASE iliyoko Kampala, Uganda alikokuwa akipatiwa matibabu baaada ya kupigwa vibaya na watu ambao bado hawajajulikana.