Polisi yakanusha mwanamke kujifungua nje ya kituo
Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro limekanusha taarifa zinazozagaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusu kujifungua nje ya kituo cha polisi, mtuhumiwa (Amina Mbunda) mkazi wa Kisanywa tarafa ya Mang’ula mkoani humo na badala yake alijifungua wakati akiwa njiani kuelekea hospitali.