Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akijibu kero mbalimbali za wananchi wa kijiji cha Kisumba katika wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa baada ya msafara wake kusimamishwa na wananchi hao.
Msafara wa Waziri wa Maliasili, Dkt. Hamisi Kigwangalla umesimamishwa na kundi kubwa la wananchi wa kijiji cha Kisumba kilichopo wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa wakiwa na mabango yanayoeleza kero zao mbalimbali.