Waziri Ndugulile agoma kuzindua majengo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amegoma kuzindua majengo ya chuo cha Afya cha waganga wasaidizi mkoani Mara kutokana na kutoridhishwa na matumizi ya fedha ya kiasi cha shilingi milion 500 kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi huo.