Fatuma Issa wa Kilimanjaro Queens kwenda Ulaya
Mlinzi mahiri wa timu ya soka ya taifa ya wanawake na ile ya Tanzania bara pamoja na klabu ya Evergreen Queens, Fatuma Issa Maonyo, anatarajia kwenda nchini Sweden kucheza soka la kulipwa kwenye moja ya klabu zinazoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini humo.