Manula afunguka ubora wa Amunike na ndoto za AFCON
Mlinda mlango namba moja wa Tanzania, Aishi Manula, amefunguka juu ya ubora wa kocha wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania 'Taifa Stars' kwa kusema ubora wa kocha Emmanuel Amunike utaisaidia Stars kucheza fainali za AFCON 2019.