Ubunge wa Mtolea Temeke wapingwa
Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC), imetangaza kupokea rufaa ya Ngulangwa Mohamed Mshamu, wa CUF, akipinga kutangazwa kushinda bila kupingwa kwa Mgombea Ubunge wa Chama Cha Mapinduzi CCM, katika Jimbo la Temeke Abdallah Mtolea.

