Aliyezuia kitanda kusafirishwa apewa adhabu
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), imeeleza kumchukulia hatua za kinidhamu mmoja wa Maafisa wake wa Misitu wa Wilaya ya Korogwe, aliyeonekana kwenye kipande kifupi cha Video iliyokuwa ikisambaa mitandaoni akibishana na abiria aliyekuwa akisafirisha vitanda viwili vya mbao.

