"Vumilieni, nazijua shida zenu" - Rais Magufuli
Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, leo Julai 16 amefanya ziara ya kushtukiza katika gereza la Butimba Jijini Mwanza, ambapo amesikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wafungwa pamoja na askari magereza.