Bosi UDART na mkewe warudishwa rumande
Kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya huduma za Usafirishaji wa Mabasi Yaendayo kwa Haraka (UDART), Robert Kisena na Wenzake wanne, imepigwa tena kalenda katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, hadi itakaposikilizwa tena Julai 15, 2019 baada ya upelelezi wa kesi hiyo kutokamilika.