Polisi yamkana Maalim Seif, Zitto azungumza
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Thobias Sedeyoka amesema jeshi hilo halijavunja kongamano lililoandaliwa na kamati ya maridhiano Zanzibar na kuhudhuriwa na Mshauri Mkuu wa Chama cha ACT - Wazalendo, Maalim Seif Sharrif Hamadi pamoja na kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe.