''Hata mkiniua leo hamuwezi kupona'' - Mpina
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ametangaza kiama kwa wavuvi haramu waliohusika katika mauaji ya watu wanne, akiwemo ofisa mfawidhi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Ukerewe yaliyotokea hivi karibuni.