Waziri Mkuu atoa onyo la mwisho kwa Mkurugenzi
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, ametoa onyo kali kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Geoffrey Mwangulumbi pamoja na Mwekahazina wa Manispaa hiyo, Pascal Makoye, ambapo amewataka wabadilike na waache kugombana na badala yake watekeleze majukumu yao.