Tanzania kuiuzia mahindi nchi ya Kenya
Naibu Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema, Serikali itaiuzia nchi ya Kenya mahindi tani milioni moja katika kipindi cha mwaka mmoja, baada ya msimu wa mvua kugoma nchini humo hali inayotishia kuwepo kwa upungufu wa chakula.