Matapeli wa 'tuma kwa namba hii' waendelea kunaswa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema jeshi la polisi mkoani humo linawashikilia watu takribani tisa wanaojihusisha na utapeli kwa njia ya simu kupitia jumbe mbalimbali za maandishi.