Polisi DSM yataja sababu ya kumkamata mwandishi
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema Jeshi la Polisi linamshikilia kwa mahojiano mwandishi wa habari Erick Kabendera aliyekamatwa Julai 29, 2019 nyumbani kwake maeneo ya Mbweni Jijini Dar es Salaam.