Katavi: Familia yagongwa na gari, mmoja afariki
Mtoto wa miezi 8 Anastazia Muli, Mkazi wa Kijiji cha Kasekese wilayani Tanganyika amefariki Dunia, huku wawili wakijeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea mkoani Katavi, ikihusisha gari yenye namba za usajili T-392, AXR aina ya Toyota Hiace kwa kuwagonga watu hao wa familia moja.