Serengeti : Ng'ombe waibiwa kwa Bodaboda
Baadhi ya Madiwani katika Wilaya ya Serengeti, wamelalamikia kuwepo kwa matukio ya wizi wa mifugo, kunakofanywa na baadhi ya wananchi katika Wilaya hiyo, hali inayopelekea baadhi ya wananchi kutojikita zaidi kwenye shughuli za maendeleo, badala yake wanakesha kulinda mifugo yao.