''Simfundishi Mzee ila sitaki kuwa mnafiki'' - JPM
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameshangazwa na namna Rais wa Uganda Yoweri Museveni, anavyoendelea kumng'ang'ania Kamishina wa Mamlaka ya Mapato wa nchi hiyo (URA), ambaye anaonesha kukwamisha ujenzi wa bomba kubwa la Mafuta kutoka Ohima kuja Tanzania.

