Rais wa Uganda kuwasili nchini kibiashara
Rais wa Uganda Yoweri Museveni, anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania mapema mwa mwezi Septemba, ambapo atakutana na kufanya majadiliano ya fursa za uwekezaji miongoni mwa nchi hizo mbili na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.