Moro : Maji yasababisha wanaume kuachiwa watoto
Baadhi ya wanaume katika Kijiji cha Fulwe, mkoani Morogoro wanaachiwa watoto na wake zao kwa ajili ya kuwatunza hasa inapofika nyakati za usiku, kutokana na wake zao kulazimika kuamka nyakati hizo na kwenda kutafuta maji, kwa ajili ya matumizi ya majumbani.
