Wasiojulikana wachoma moto nguzo za umeme
Naibu waziri wa Nishati, Subira Mgalu ameeleza kusikitika kwa kitendo cha baadhi ya wananchi, ambao hawakujulikana kwa mara moja , kuchoma moto nguzo (60) za umeme, katika eneo la Kata ya Pande wilayani Kilwa, mkoani Lindi.
