MOI Kutoa huduma kwa njia ya mtandao
Taasisi ya mifupa MOI inatarajia kuanza kutoa huduma kwa mfumo wa mtandao, utakaoziwezesha hospitali mbalimbali nchini kuwa na uwezo wa kutuma picha za X-ray na kusomwa na madaktari bingwa wa Taasisi hiyo na kisha majibu hayo kurudishwa kwa njia ya mtandao.

