Kampeni ya Namthamini yaleta faraja Mbeya
Kampeni ya Namthamini, inayoratibiwa na East Africa Television na East Africa Radio yenye lengo la kumuwezesha mtoto wa kike asikose masomo shuleni akiwa katika hedhi, imeendelea kutoa msaada wa taulo za kike (Pedi) kwa shule mbalimbali nchini ambapo awamu hii imefika Mbeya.

