"Tunadhibiti watu wasiibiwe, wasivuke" - RPC Tanga
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Edward Bukombe, amesema kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo linaendelea kuimarisha usalama kwa abiria wote, waliokwama kuendelea na safari baada ya maji kujaa juu ya daraja ili kuepusha madhara makubwa hususani wale ambao watalazimisha kuvuka.

