Kigogo wa serikali anaswa akiomba rushwa Mil 12
Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), mkoani Kagera, itamfikisha mahakamani kaimu meneja mkuu wa kampuni ya ranchi za taifa (NARCO) Prof. Philemon Wambura, kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya shilingi milioni 12, kutoka kwa mtu aliyetaka kumpatia kitalu cha ufugaji.

